NJOLE : SERIKALI IPO KATIKA MCHAKATO WA KUSIMAMIA MATUMIZI YA AI
Na Mwandishi wetu,
MWANDISHI Mkuu wa Sheria, Onorius Njole amesema kuwa Serikali ipo katika mchakato wa kutengeneza mfumo wa kisheria kwa ajili ya kusimamia matumizi ya teknolojia ya Akili Mnemba (AI)
Njole ameyabainisha hayo katika maonesho ya 49 kimataifa ya biashara ya Sabasaba(DITF) yanayoendelea .
Amesema mfumo maalumu kwa ajili ya kusimamia matumizi ya IA unaandaliwa na Serikali na mara tu baada ya kukamilika miswada ya sheria utaandaliwa .
Katika hatua nyingine Njole amesema kuanzia mwezi Agusti mwaka huu toleo la sheria zilizotafsriliwa kwa lugha ya kiswahili litaanza kutolewa.
Amesema kutafsiliwa kwa sheria kutasaidia wananchi wa makundi yote kuelewa na kufuata sheria kwa urahisi.
"Agizo hili lilitolewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kama sehemu ya maboresho ya Sheria nchini"amesema
Aidha amesema sambamba na mchakato wa kutafsiri sheria, Ofisi ya mwanasheria Mkuu imeendelea kufanya mabadiliko makubwa sheria hili kuhakikisha sheria zilizopo zinatekelezeka kwa ufanisi na kuwafikia wananchi Kwa lugha sahihi inayoeleweka.
Kwa upande wake Mwandishi Msaidizi Mkuu wa Sheria, Rehema katunga amesema zinazorebishwa zimeanza kutumika rasmi Julai 1,2025 .
Amesema sheria za awali ambazo hazijafanyiwa marekebisho hazitatumika tena .


Comments
Post a Comment