OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA KWA TAASISI ZA UMMA



Na Mwandishi wetu

OFISI ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imesema  itaendelea kuboresha Ushauri kwa Taasisi za Umma wakati wa kuingia mikataba mbalimbali ili kuwa na Mikataba iliyobora kutimiza malengo ya Serikali ya kuwa na mikataba inayotekelezwa vizuri na kuwanufaisha Wananchi.

Hayo yamebainishwa na  Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Samwel Maneno katika Maonesho ya Kimataifa ya 49 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.



"Tunaendelea kuzipa ushauri Taasisi za Umma ili kuwa na ubora wa kufanya biashara pia kwenye utekelezaji wa Mikataba hiyo unafanyika kwa mujibu wa Makubaliano" amesema 

Aidha, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inayatumia maonesho hayo katika kutoa Ushauri wa Kisheria, Kushughulikia Malalamiko, Utatuzi wa Migogoro na Elimu ya Sheria hususani masuala yaliyofanyiwa Urekebisho toleo la Mwaka 2023 zilizoanza Julai 1, 2025.

"Sheria zilizofanyiwa urekebisho zimezinduliwa na zimeanza na kitu kizuri ni kuwa kati ya sheria 446 sheria 300 zinapatikana kwa lugha ya kiswahili".ameeleza

Katika hatua nyingine Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali alitembelea mabanda ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria pamoja na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo, kuona shughuli zinazotekelezwa na Taasisi katika maonesho hayo.

Maonesho ya Sabasaba 2025 yamezinduliwa rasmi Julai,7 2025 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambapo maonesho yanatarajiwa kumalizika  Julai,13 2025.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA