PURA MBIONI KUJENGA VISIMA VITATU VYA GESI ASILIA MTWARA
Na Mwandishi wetu
MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), umesema kwa sasa upo katika mchakato wa kuchimba visima vitatu vya gesi asilia Mkoani Mtwara unaotarajia kuanza Novemba mwaka huu.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa PURA ,Mhandisi Charles Sangweni alipotembelea katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam(DITF) maarufu lama Saba Saba alipotembelea katika banda la PURA na taasisi nyingine mafuta na wizara ya nishati.
Amesema maandalizi ya uimbaji wa visima hivyo vitatu vya gesi asilia umelega kuongeza mafuta ya nishati hiyo.
"Katika kudumu 10 ambayo yanapatiwa tenda ya kufanya kazi kwenye miradi hii,PURA itahakikisha zaidi ya kampuni sita zitakuwa kitanzania ili kuhakikisha watanzania wanafaidika na miradi hiyo"amesema
Pia amesema katika uchimbaji huo Shirika la Petroli Nchini (TPDC ) limeshiriki kwa asilimia 40% huku asilimia 60% zilizobaki zinafanywa na kampuni nje ya nchi.
"Kazi zote ambazo kutuma kwa mashuhuri ya kitanzania zinafanywa na Watanzania kwa kuwawezesha sasa hivi kumekuwa na msaada wa kusaidia wanatalaam wa masuala ya mafuta na misaada kozi z masomo hayo," amesema amesema.
Aidha Mhandisi Sangweni ameipongeza Tantrade kwa Mapinduzi makubwa yaliofanyika katika maonesho ya Sabasaba 2025 ya kulinda mambo yote yanafanyika kidigitali.
Amesema ushiriki wa Wananchi kufika katika maonesho hayo umekuwa ni mkubwa zaidi huku wengi wao wakijitokeza kutembelea katika Banda la PURA.



Comments
Post a Comment