PURA, ZPRA ZAJIVUNIA MIAKA MITATU YA MASHIRIKIANO

 



Na Mwandishi wetu

MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) ya Tanzania Bara na Mamlaka ya Uthibiti, Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta Zanzibar (ZPRA) ya Zanzibar zimeeleza kujivunia mafanikio yaliyopatikana tangu taasisi hizo ziliposaini hati ya Makubaliano (Memorandum of Understanding - MoU) mwaka 2022.

Hayo yameelezwa Julai 01, 2025 Jijini Dar es Salaam katika kikao kilichohusisha menejimenti za PURA na ZPRA kwa lengo la taarifa ya utekelezaji wa MoU kwa mwaka wa fedha 2024/25.



Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa PURA,  Charles Sangweni amesema kuwa tangu kuanza kutekelezwa kwa MoU, Taasisi za PURA na ZPRA zimefanikisha masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujengeana katika eneo la udhibiti wa shughuli za utafutaji, uendelezaji na mafuta wa mafuta na vyanzo asilia.

“Ni jambo la kujivunia kuona hali ya kutekeleza wa MoU baina yetu umeendelea kuimarishwa hadi mwaka na tumeweza masuala masuala mengi kupitia MoU hii” amesema Sangweni.



Kwa upande wake, Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZPRA,  Mohammed Said amesema miaka mitatu ya MoU imekuwa na manufaa kwa taasisi hiyo hususan katika eneo la kujenga uwezo.

Kusainiwa kwa MoU, PURA na ZPRA zimeweza kubadilishana ujuzi na kujengeana uwezo katika maeneo mbalimbali pamoja na data za petroli, gharama za gharama za uandaaji wa sheria, kanuni na miongozo.

Maeneo mengine ni mamlaka na usimamizi wa shughuli za mkondo wa juu wa petroli na ushiriki wa wananchi katika shughuli hizo.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA