TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUTUMIA MAONESHO YA 77 KUJITAGAZA

 



Na Mwandishi wetu

OFISI ya Msajili wa Hazina imetoa rai kwa taasisi ya kutumia maonesho ya 49 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba kama jukwaa la kutangaza huduma zinazotolewa na serikali.

 Akizungumza katika maonesho hayo Kaimu Mkuu Kitengo Cha Mawasiliano kwa umma kutoka ofisi ya msajili wa hazina Sabato Kosuri kwenye Banda la ofisi hiyo maonesho ya sabasaba ambapo amesema wananchi ndio taasisi za umma na hivyo wanahaki ya kujua ukweli na unaoendelea na serikali. 

Amesema kwamba Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imewekeza kiasi cha Shilingi trilioni 86.25 katika taasisi ya umma na kampuni ambayo Serikali ina umiliki wa hisa ambapo kiasi hicho shilingi trilioni 83.33 zimewekezwa kwenye taasisi 152 ambazo serikali ina hisa nyingi, huku Shilingi trilioni 2.82 zikiwekwa kwenye kampuni 56 ambazo serikali inamiliki. 


Aidha amesema Maonesho ya biashara ya Sabasaba ni mwendelezo wa tafsiri ya ndoto ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuongeza ufanisi wa taasisi za umma lengo likiwa ni kuleta tija na rejesho halisi la biashara katika taasisi za umma.  

Kosuri amebainisha kuwa ushiriki wa Ofisi ya Msajili wa Hazina na taasisi inazozisimamia katika maonesho ya Sabasaba utawapa fursa kwa wadau na wananchi kwa kuuliza maswali na kutoa maoni.




Hata hivyo Kosuri amehitimisha kwa kuwakaribisha wadau mbalimbali na wananchi wote katika banda namba 39 la Ofisi ya Msajili wa Hazina lililopo katika ukumbi wa Kilimanjaro.


Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA