TASAC YATOA ELIMU YA USALAMA WA USAFIRI MAJINI SABASABA




Na Mwandishi wetu

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema litaendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya  usalama wa usafiri majini jinsi  unavyochagia katika uchumi wa Nchi.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa bodi ya wakurungezi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC ) Naodha Mussa Mandia alipotembelea Banda la TASAC lililopo katika Maonesho ya 49 ya  Biashara ya Kimataifa yanayoendelea sabasaba wamekuwa wakitoa elimu kwa jamii juu ya usafiri wa majini unavyochagia katika uchumi wa Nchi .

Amesema TASAC  ina jukumu la kudhibiti na kusimamia usalama,ulinzi wa usafirishaji majini ambao ni kiungo kikuu katika kukuza uchumi.





"TASAC inayo majukumu mawili moja la Udhibiti na lingine kuamasisha watu kushiriki katika ulinzi na usalama na usafiri na usafirishaji kwa njia ya maji"amesema

Amesema majukum mengine ya TASAC ni pamoja na kuhakikisha meli zote zinazotia nanga kwa ajili ya kuleta bidhaa mbalimbali nchini zinakuwa salama pamoja na kulinda mazingira ya bahari.

Akizungumzia kuhusu maonesho ya Sabasaba amesema TASAC inashiriki katika maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi inavyohakikisha usalama na ulinzi wa bandari zote nchini.




Katika hatua nyingine Kapteni Mandia  amesema 
hali ya usalama wa bahari ni shwari na TASAC imekuwa ikishirikiana na vyombo usalama katika maeneo hayo kupitia vyombo vya ulinzi na usalama

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA