TUNAWEZA KUZUIA ASILIMIA 80 YA VIFO NCHINI TUKIBADILI MTINDO WA MAISHA-DKT.BITEKO

 



Asisitiza kuhusu mazoezi ya mwili ili kujikinga na maradhi yasiyoambukiza*

Apongeza NBC Dodoma Marathon kuiunga mkono Serikali mapambano dhidi ya Saratani ya Shingo ya kizazi na kusomesha Wataalam wa Afya.

Napongeza Kampeni ya MTU NI AFYA inayohamasisha Watanzania kufanya mazoezi

NBC Dodoma Marathon yawezesha matibabu ya Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake 4800; mafunzo kwa Wakunga 100 na kuchangia ujenzi wa wodi


Na Mwandishi wetu 

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema kuwa asilimia 80 ya vifo nchini wanaweza kuzuilika endapo Watanzania wataamua kubadilisha maisha na kuwa na matokeo ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara.

 Amesema hayo mapema leo Julai, 27, 2025 jijini Dodoma akimwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kilele cha msimu wa Sita wa NBC Dodoma Marathon 2025 ambayo imelenga kukusanya fedha kwa ajili ya kuokoa afya ya mama na mtoto.

“Taarifa ya Shirika la Afya Duniani ya mwaka 2022, inaeleza kuwa, mazoezi ya mara kwa mara kama vile kukimbia, yana uwezo wa hatari ya ugonjwa wa moyo kwa zaidi ya asilimia 35.Vile vile, mazoezi ya kusaidia kujikinga na magonjwa mengine yasiyoambukiza kama shinikizo, shinikizo la damu, ugonjwa na magonjwa mengi.” Ameeleza Dkt. Biteko



Kwa upande wa Tanzania, Dkt. Biteko amesema asilimia 33 ya Watanzania watu wazima wazima wenye uzito uliopitiliza na asilimia 28 wana shinikizo la damu ambapo amechangia kuwaeleza hayo zaidi ya asilimia 40 ya vifo vya mapema lakini asilimia 80 ya vifo hivyo basi kubadili mtindo wa maisha.   

Dkt. Biteko ameipongeza Benki ya NBC kupitia NBC Dodoma Marathon kwa kuunga mkono Serikali katika nyanja mbalimbali kwani Sekta ya Afya mwaka 2025 Marathon hiyo imelenga kuleta mapato ya Saratani ya kizazi kwa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

Pia, imetoa ufadhili wa masomo ya Wakunga kupitia ya Benjamin Mkapa ili kusaidia taasisi ya mama na mtoto wakati wa uzazi na kutoa ufadhili kwa mafunzo ya Wauguzi Maalum wa kusaidia watoto wenye changamoto za usonji (Autism), kwa masomo na AMREF Afrika.



Vilevile, Dkt. Biteko amesema tangu NBC Dodoma Marathon kuanzishwa mwaka 2020 imekuwa ni moja ya vile vile vya kujenga mshikamano, uzalendo wa kweli na kutatua matatizo mbalimbali katika jamii changamoto. 

Dkt. Biteko ameipongeza NBC Dodoma Marathon kwa kuendelea kuimarishwa kwani mwaka 2024 ilihusisha washiriki 8,000 na mwaka huu imekuwa na washiriki zaidi ya 12,000 sawa na gazeti zaidi ya asilimia 50. 

Vile vile, mwaka 2024 NBC Dodoma Marathon ilikusanya kiasi cha Shilingi Milioni 300 huku mwaka 2025 ikikusanya kiasi cha Shilingi Milioni 700 sawa na gazeti la asilimia 133.33.

Amesema kuwa, Serikali itaendelea na wadau kama NBC ambao wameendelea kutumia mashindano ya mbio za afya za wananchi na masuala mbalimbali katika kuokoa afya zachangia.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko ametoa rai kwa Wizara ya Afya, Serikali za Mitaa, zana ya kiraia, Sekta binafsi na wananchi wote kufanya mbio na mazoezi kuwa sehemu ya maisha ya kila siku ili kuweza kujikinga na matatizo ya afya ambayo wananchi wanaweza kuyapata.

“Nitashukuru sana kusikia kila Taasisi imetenga kwa uchache siku moja kwa mwezi ili kuwa na mazoezi ya pamoja, hii kuimarisha afya zetu na kujenga Taifa Imara.” Amesisitiza Dkt.Biteko     

 Vilevile ameipongeza Wizara ya Afya, kwa Kampeni ya MTU NI AFYA inawahamasisha Watanzania kufanya mazoezi angalau dakika 30 kila siku, kula lishe bora, kupima afya mara kwa mara na kujiepusha na tabiashi.

Kwa upande wake, Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema mbio za NBC Dodoma Marathon zimekuwa kivutio kwa wanamichezo wengi kushiriki kutokana na kuandaliwa vizuri ambapo amesema kuwa Wizara hiyo itaendelea kuiunga mkono benki ya NBC katika maandalizi ya mbio hizo ambazo zimekuwa na matokeo chanya.


Amesema Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo itaendelea kuweka mazingira mazuri ya wananchi kushiriki michezo mbalimbali na kujenga viwanja vya michezo katika maeneo mbalimbali ya Arusha, Dodoma na Dar es Salama ili kuwezesha uimarishaji kimichezo na kiafya.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi alisema NBC Marathon imekuwa ni moja ya alama za sekta binafsi katika kuwekeza kwenye sekta ya afya na nyinginezo, akieleza kuwa katika kipindi cha mbio hizo zimefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi 1, ambazo zimekuwa na mchango mkubwa katika Sekta ya Afya.

Ametaja mafanikio ya marathon hiyo kuwa ni pamoja na kutoa elimu na uhamisho wa Saratani ya kizazi cha Wanawake zaidi ya 200,000 na kufadhili matibabu kwa wagonjwa 4,800 waliogunduliwa na kansa hiyo katika Hospitali ya Ocean Road.

Amesema, NBC Dodoma Marathon imetoa ufadhili kwa Wakunga 100 katika chuo cha Wakunga Morogoro kwa taasisi ya Benjamin Mkapa huku lengo likiwa ni kufadhili wakunga 500 ifikapo 2028.

Pia ameeleza kuwa, NBC Dodoma Marathon imechangia ujenzi wa Wodi maalum ya Wanawake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na maeneo mengine katika maendeleo ya sekta ya afya. 

Amesema msimu wa sita wa NBC Dodoma Marathon umehusisha wakimbiaji 12,000 na wamefanikiwa kukusanya shilingi milioni 700 kwa ajili ya afya ya mama na mtoto ikilenga uchunguzi wa kizazi cha wanawake 10,000, kutoa ufadhili kwa wakunga 100 na mpango mpya wa masomo kwa wauguzi 100 watakaoshughulika na watoto wenye changamoto.  


NBC Dodoma Marathon 2025 iliyokuwa na kaulimbiu ya Kata Wese Okoa Maisha imehusisha wanariadha kutoka nje ya nchi ambapo washindi wamepewa zawadi ya jumla ya shilingi milioni 80. Aidha imekabidhi pikipiki 10 kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA