WARATIBU, WASIMAMIZI NA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA JIMBO WAPATIWA MAFUNZO JIJINI ARUSHA .



Na Mwandishi wetu, ARUSHA

WARATIBU wa uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo wamekutana jijini Arusha kwa siku tatu kwa ajili ya mafunzo ikiwa ni maandalizi ya kutekeleza kazi na jukumu lililo mbele yao.

Akifungua mafunzo hayo Mjumbe wa Tume huru ya Taifa ya uchaguzi , Dkt.Zakia Abubakar amesema kuwa, wameteuliwa kwa mujibu wa Sheria na tangu tarehe uteuzi wao wana wajibu wa kuomba kuomba na kuratibu uchaguzi wa Rais, wabunge, madiwani kwa Tanzania bara kwa niaba ya Tume katika uteuzi.

Amesema kuwa dhamana waliyopewa na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi ni muhimu na muhimu kwa mustakabali wa Taifa letu hivyo wanategemewa kwa kuzitambua utendaji wao.




Aidha amewataka kuwajibika ipasavyo kipindi katika alichagua cha utumishi wao wa Tume hadi hapo watakapokamilisha jukumu hilo la uchaguzi mkuu.

Amesema kuwa,mafunzo hayo yanajumuisha washiriki 86 kutoka mikoa ya Arusha ,Manyara ambao ni waratibu wa uchaguzi wa mikoa,wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo,maafisa uchaguzi na ununuzi.

“Mafunzo haya yanafanyika kwa wakati mmoja katika mikoa ya Dar es Salaam,Mbeya,Mwanza,Shinyanga,Ruka na Kusini Pemba .”amesema .

Amewasilisha kuwa, kumi na mbili zitawasilishwa ambapo pamoja na mambo mengine watapata fursa ya kubadilishana ujuzi na uangalizi wa uchaguzi katika maeneo yao na namna ya kupokea .na changangamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika hatua zote za uchaguzi.

” Natumia nafasi hii kuwaasa pamoja na uzoefu ambao baadji yenu mnao katika uendeshaji wa uchaguzi msiache kusoma katiba,Sheria, kanuni,taratibu,miongozo na fuateni na tekelezeni maelekezo mbalimbali yatakayokuwa yanatolewa na Tume .”amesema. 

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA