WAZIRI KIKWETE AIPA TANO OFISI YA MSAJILI WA HAZINA




Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete, ameipongeza Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa mageuzi makubwa iliyofanya katika bodi ya umma. 

Kikwete alitoa pongezi hizo Julai 4, 2025, alipotembelea banda namba 39 (Ukumbi wa Kilimanjaro) katika maonesho ya 49 ya biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

“Tunaishukuru Ofisi ya Msajili wa Hazina chini ya uongozi imara wa Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, kwa kuwezesha taasisi za umma kuongeza ufanisi wao,” amesema Kikwete.





Aliongeza: “Wote ni mashahidi, katika uongozi wa awamu ya sita chini ya Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan, tumeshuhudia mabadiliko makubwa ya kiutendaji katika taasisi za umma.”

Ofisi ya Msajili wa Hazina imewezesha kuimarika kwa kampuni ya umma yaliyokuwa na mitaji hasi na yaliyokuwa yanapata hasara mfululizo, ambapo sasa yameweza kupokea na utegemezi wa ruzuku ya Serikali na kufanikiwa kutoa gawio. 





Baadhi ya mashirika hayo ni pamoja na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), ambapo mchango wake katika Mfuko Mkuu wa Serikali ulikuwa Sh10.5 bilioni katika mwaka wa fedha 2024/25. 

 Pia, katika orodha ya mashirika ambayo sasa yanajiendesha kwa shirika la Taifa la Madini (STAMICO), Shirika la Umeme (TANESCO), na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) 





 Kikwete amesema serikali itaendelea kuiunga mkono ofisi ya Msajili wa Hazina katika kulinda safari ya mageuzi inafanikiwa.

“Endeleeni kufanya kazi kwa bidii na pale ambapo kuna mambo mnataka yabadilike katika taasisi ambazo ziko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, hesabuni mmepata ushirikiano kutoka kwetu,” amesema Kikwete. 

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri, alisema kumekuwa na kubwa la ufanisi kwenye baadhi ya matokeo kutokana na mageuzi yaliyofanyika na yanayoendelea katika majadiliano ya umma. 

“Ufanisi umeimarika kwa kiasi kikubwa, mfano mzuri tunauona kwenye Mamlaka ya Bandari,” amesema Kosuri.

Kwa mwaka huu wa fedha hapo, pamoja na mchango kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali kutoka Sh155.7 bilioni mwaka 2023/24 hadi Sh181 bilioni mwaka 2024/25, matumizi ya kawaida kwa ajili ya uendeshaji wa bandari pia yamepungua kwa kiasi cha Sh505.59 bilioni sawa na ufanisi wa asilimia 46.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA