WAZIRI MKUU MAJALIWA AKABIDHI TUZO YA UMAHIRI KWA MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA NISHATI.



Ni kufuatia Umahiri wa masuala ya Mawasiliano kwenye Maonesho ya Osaka Expo 2025

 Ampongeza kwa kuwa Kiongozi wa mfano wakati wa Mkutano wa Biashara na Uwekezaji na Utalii Osaka Expo 2025

Na Mwandishi wetu

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa leo tarehe 13 Julai, 2025 amemkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Nishati, Neema Chalila Mbuja tuzo ya umahiri mchango wake alioutoa wakati wa Maonesho ya Dunia ya Biashara ya Osaka nchini Japan kwa upande wa Mawasiliano na kuitangaza nchi.

Majaliwa amempongeza Mbuja wakati wa kilele cha Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba 2025.




Sambamba na hilo Majaliwa amempongeza Mbuja kwa kuwa muongozaji wa shughuli na kuwa mahiri wakati wa Kongamano la Kimataifa la Biashara, Uwekezaji na Utalii kwenye Maonesho ya Osaka Expo 2025.

Kwa upande wake Mbuja amemshukuru Majaliwa kwa kukabidhi tuzo hiyo na mamlaka ya Maendeleo ya Biashara TANTRADE na kuahidi kuendelea kuitangaza Wizara ya Nishati Kimataifa






.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA