WAZIRI RIDHIWANI ATOA WITO KWA VIJANA KUCHAGAMKIA FURSA ZILIZOPO
Na Mwandishi wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete ametoa wito kwa vijana kuchagamkia fursa mbalimbali ikiwemo mikopo ya uwezeshaji wananchi.
Kikwete ametoa wito huo alipotembelea Banda mamlaka la Ofisi ya Waziri Mkuu lilipo katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya sabasaba .

"Serikali imeendelea kupata fedha za hisa za kampuni mbalimbali yananufaika kwa mfano kupitia sheria ya Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma (PPRA) imeelekeza asilimia 30 ya manunuzi yote ya umma ipelekwe katika kusaidia fedha za vijana, akinamama na wenye ulemavu"amesema
Aidha amesema upo Mfuko wa kusaidia watu wenye ulemavu..pamoja na mfuko wa vijana na uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Aidha amewataka waziri wa habari na watumishi wa umma na wadau mbalimbali kuzidi kupaza sauti juu ya mifuko ya mifuko na faida zake.
Katika hatua nyingine amezielekeza Idala na Taasisi za Serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi hususani ili waweze kupata fursa za mikopo na uwezeshaji wananchi.
"Maelekezo yetu ni kwamba Idala zote , Taasisi zote kusaidia kwamba elimu inakuwa muhimu zaidi .. Serikali ya awamu ya sita inayoongoza na Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mambo yaliofikiwa ni pamoja na kufanya watu wapate elimu ili waweze kujinusuru katika maeneo mbalimbali.
Katika wakati mwingine Kikwete ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi wote kusaidia wanalinda katika kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanya kazi baadaye Octoba mwaka huu.

Comments
Post a Comment