BoT ACADEMY NA WFP WAUNGANA KUWAJENGEA VIJANA UWEZO WA ELIMU YA FEDHA.





Na Mwandishi wetu 

CHUO cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT Academy) kimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwa lengo la kuwajengea uwezo wa elimu ya fedha vijana kupitia Mradi wa Vijana Kilimo Biashara (VKB).

Hafla hii ya utiaji saini imefanyika Julai 31, 2025, katika ofisi za BoT jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania,  Emmanuel Tutuba.

Akizungumza katika hafla hiyo, Gavana Tutuba ameishukuru na kuipongeza WFP kwa serikali ya Tanzania katika kuwawezesha vijana wanaofaika mradi huo kupata maarifa ya kifedha yanayowawezesha kuboresha maisha kupitia biashara.



"Leo tumesaini rasmi ushirikiano wa Mradi wa Vijana Kilimo Biashara, ambao unatekelezwa kwa pamoja na BoT Academy Mwanza na WFP. Wenzetu wa WFP wamekubali kufadhili elimu ya fedha kwa vijana katika mikoa saba hapa nchini. Mikoa hiyo ni Dodoma, Arusha, Tabora, Singida, Manyara, Simiyu na Shinyanga." amesema Gavana Tutuba.



Ameeleza kuwa Chuo cha Benki Kuu kitatoa elimu ya fedha kwa vijana ambao watawezeshwa na WFP kupitia mradi wa VKB ili waweze kupata fedha zao kwa ueledi kutumia kutuma taarifa ya bodi.

Gavana Tutuba alizungumza kuwa kwa kufanya hivyo vijana ambao wamepewa elimu hiyo wataweza kufanya shughuli zao za kilimo kwa kujikita zaidi kwenye bora wenye tija kupitia kilimo cha mboga, mtama pamoja na alizeti. 

Aidha, Gavana Tutuba amebainisha kuwa Serikali itaendelea na mbalimbali ili kusaidia elimu ya fedha inawafikia mikopo yote ya jamii, wakiwemo wanawake, watu wenye ulemavu, wavuvi, na wajasiriamali ambao wana utafiti unaonesha majina hayo hayajafikiwa na elimu ya fedha ya kutosha.


Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mkazi wa WFP, Christine Mendes amesema Mradi wa VKB nchini, unaofadhiliwa na Mastercard Foundation, unalenga kuwapatia vijana ujuzi na rasilimali muhimu ili kuboresha uchumi endelevu.

Mendes amesema tangu kuanza kwa mradi huo mwaka 2022, zaidi ya vijana 83,000 wameshanufaika – asilimia 70 kati yao wakiwa wanawake. 

Ameongeza kuwa ni kuwafikia jumla ya vijana 115,000 ifikapo mwaka 2027, huku kupitia huo, WFP ikitoa ufadhili wa dola za Marekani 100,000 (sawa na zaidi ya shilingi milioni 250) kwa ajili ya mafunzo ya fedha za kifedha, kuweka akiba, kuweka fedha na fedha za kilimo chenye tija.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA