CCM KUZINDUA HARAMBEE YA KITAIFA KUCHANGIA KAMPENI.

 



Na Mwandishi wetu

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesema CCM imeweka lengo la kukusanya Shilingi Bilioni 100 kupitia harambee ya kitaifa itakayozinduliwa rasmi leo Agosti 12, 2025 katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Dkt Nchimbi ameyabainisha hayo wakati akizugumza na wahariri na Waandishi wa habari katika ofisi ndogo ya CCM Makao Makuu, Lumumba mkoani Dar es Salaam, Agosti 11, 2025

Dkt Nchimbi amesema amesema watayarisha harambee hiyo umetokana na hamasa kubwa iliyojitokeza kwa wanachama wa CCM kutaka kuchangia kampeni.




"Kwa wakati ulitokea tukio kubwa kwa wanachama wa CCM kutamani kuchangia mchango wa kampeni. Kutokana na hamasa hiyo, kama Kamati Kuu tumeamua sasa kuwashirikisha wanachama wetu katika uchangiaji  saa 11 jioni katika ukumbi wa Mlimani City,"

Aidha, Dkt. Nchimbi ameeleza malengo ya kuchangia, ambapo amesisitiza kuwa;

“Tunachokusudia kiwango cha kawaida ni Bilioni 100. Wanasiasa kokote walipo wajue hiyo ndiyo target tunayokusudia.”

Vilevile, Dkt. Nchimbi amefungua milango kwa vyama vingine kuchangia katika kampeni hiyo ambapo amesema kuwa;

"Kuhusu vyama vingine, tutafarijika sana vikichangia, kwa sababu haihitaji ushahidi wa polisi kujua CCM inatumikia Watanzania na vyama vyote."

Akizungumzia kuhusu mamlaka wa fedha haramu, Dkt. Nchimbi amesema “Jitihada yetu kubwa sisi kama CCM ni kuepusha kuwa Serikali, kwa hiyo sisi siyo taasisi ya uchunguzi wa fedha haramu.

Harambee hiyo kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA