DKT. KIKWETE: UTEUZI WA DKT SAMIA ULIFUATA TARATIBU ZA CCM.
Na Mwandishi wetu
MWENYEKITI mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Kikwete amesema mchakato wa kumteua Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho Dkt. Samia Suluhu Hassan ulifuata utaratibu wa siku zote, na kwamba kwa wale walioona mchakato haukufuata taratibu hawafahamu taratibu za chama hicho.
Dkt. Kikwete amesema hayo mapema leo Agosti 28,2025 wakati akitoa salamu katika uzinduzi wakampeni za uchaguzi wa CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, unaofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam.
Amesema anashangaa kuona watu wanabeza uteuzi huo wakati wengine walishiriki katika michakato ya teuzi za awamu wa awamu ambao wanafanana na mchakato uliofuatwa kwa awamu hii.
Dkt. Kikwete ametumia jukwaa hilo kumpongeza Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza kwa kishindo miradi mbalimbali iliyoachwa na utangulizi wake Hayati Dkt. John Magufuli, ambapo pia ametekeleza ilani ya CCM kwa kishindo kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika kila sekta.
Dkt. Kikwete pia amesema Dkt. Samia amekamilisha Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, huku akimuita kiongozi mwenye maono mbali mbali.

Comments
Post a Comment