INEC YAHIMIZA VYOMBO VYA HABARI KUELIMISHA NA KUAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA UCHAGUZI MKUU



Na Mwandishi wetu 

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imevihimiza vyombo vya habari nchini kuripoti kwa ripoti kwa wakati kuhusu taarifa zote zinazohusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ili kuwawezesha wananchi kushiriki katika mchakato wa uchaguzi.

Kauli hiyo imetolewa leo, tarehe 01 Agosti, 2025, jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mheshimiwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, wakati wa mkutano wa mkutano kati ya Tume na Wahariri wa Vyombo vya Habari.

Jaji Mwambegele amesema vyombo vya habari vina nafasi muhimu katika kusaidia wananchi wanapata elimu ya kupiga kura na taarifa sahihi zinazowawezesha kufanya maamuzi ya msingi kwa uhuru na kwa amani.



Aidha, amewasihi Wahariri wa vyombo vya kutumia habari majukwaa yao kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu, utakayofanyika tarehe 29 Oktoba 2025.

Amesisitiza kuwa viongozi wa Tume na vyombo vya habari ni nguzo muhimu katika uchaguzi unafanyika kwa amani na kwa kuzingatia sheria za uchaguzi.

Akitoa mada kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani amesema vyombo vya habari vina nafasi ya umuhimu wa mamlaka katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Ame kuwa, katika nchi inayodhamiria jambo kubwa kama uchaguzi, vyombo vya habari ndio msingi wa kwanza, kwani kupitia kwao, wananchi hupata taarifa sahihi, zilizofanyiwa utafiti na kuhakikiwa.



Bw. Kailima amesema kuwa katika ushirikiano wa karibu na vyombo vya habari, juhudi zote za kutoa elimu na taarifa kwa umma haziwezi kuwafikia walengwa. 

"Maana yake kila kinachotolewa na Tume hakiwezi kuwafikia wananchi iwapo vyombo vya habari havitaamua jambo hilo lifanikiwe," amesema.


Ameongeza kuwa wadau wote wa uchaguzi, vikiwemo vyama vya siasa, wanategemea vyombo vya habari kutoa taarifa zitakazowawezesha wananchi kushiriki katika mchakato wa uchaguzi.


Amesisitiza kuwa vyombo vya habari ndivyo vinavyoweza kuwa sauti ya kwanza ya kuonesha upotoshwaji wa aina yoyote unaofanywa kwa bahati mbaya au kwa makusudi kuhusu Tume na kuhusu zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.


“Tunawaomba na kupatasihi, kutumia na fursa mlizonazo nafasi kunakuwepo na taarifa za mara kwa mara za kuelezea zinazoendelea kuhusu uchaguzi,” amesisitiza Mkurugenzi wa Uchaguzi.


Aidha wahariri hao wamekumbushwa kutumia mbiu ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ambao ni “Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura” kwenye taarifa yao wanazozitoa kwa umma ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji kwa wananchi kujitokeza kupiga kura.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA