JESCA MOTTO AAHIDI MAGEUZI MAKUBWA BUYUNI
Na Mwandishi wetu
MGOMBEA udiwani wa Kata ya Buyuni, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jesca Motto, ameahidi kuleta mageuzi makubwa ya kimaendeleo katika kata hiyo endapo atachaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 15, 2025 mara baada ya kukabidhiwa barua ya uteuzi kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Chief Sylvester Yaredi, Jesca ameeleza kufarijika na imani ya chama chake kumpa ridhaa ya kugombea nafasi hiyo.
“Ulikuwa mchakato mgumu kwa sababu wagombea walikuwa wengi lakini namshukuru Mungu na chama changu kwa kunipitisha. Naahidi kuwatumikia wananchi wa Buyuni kwa nguvu zote na kushughulikia changamoto zilizopo kwa kushirikiana nao,” amesema Jesca.
Ameeleza kuwa uamuzi wake wa kugombea umetokana na kuguswa moja kwa moja na hali ya maendeleo ya Kata hiyo na kwamba dhamira yake ni kuipeleka mbele Buyuni .


Comments
Post a Comment