KAMATI KUU CCM YAMPITISHA MASABURI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KIVULE.
Na Mwandishi Wetu
CHAMA Cha MapinduziCCM (CCM) kimempitisha mwanachama wa mwaka ambaye pia aliwahi kuwa Naibu katika Meya ya Halmashauri ya Manispaa ya ilala Ojambi Didas Masaburi kuwa Mgombea ubunge wa Jimbo la Kivule jijini Dar es Salaam katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba huu
Masaburi ambaye aliongoza mchakato wa kura za maoni ya Chama hicho ametangazwa kuwa ndani Jimboni baada ya Kamati Kuu ya CCM kukaa kikao Dodoma na kuchuja majina ya ubunge wake ambao watapeperusha bendera katika Uchaguzi huo.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) CPA Amoss Makalla ametangaza majina ya ubunge katika majimbo yote ambapo jimbo la Kivule Mgombea ubunge aliyepitishwa na Chama hicho ni Ojambi Masaburi .
Baada ya kupitishwa kwa jina lake Masaburi atachukua fomu ya kugombea ubunge na kisha kuirejesha katika Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na hatimae kusubiria kampeni kwa ajili ya kuomba kura kwa wananchi katika Jimbo la Kivule.
Kwa kukumbusha tu Jimbo la Kivule ni Jimbo jipya ambalo limepatikana baada ya Tume Huru ya Uchaguzi kuligawa Jimbo la Ukonga na kupatikana majimbo mawili ambayo Ukonga na Kivule na Jimbo hilo la Kivule Mgombea wake ni Masaburi.

Comments
Post a Comment