MGOMBEA URAIS WA CHAMA CHA MAKINI AKABIDHIWA FOMU NA INEC
Na Mwandishi wetu
MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele leo Agosti 10, 2025 amekabidhi fomu ya uteuzi kwa mgombea wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano kutoka Chama cha Makini (MAKINI), Coaster Jimmy Kibonde.
Hafla hiyo imefanyika kwenye ofisi za Tume zilizopo Njedengwa Jijini Dodoma.
Kibonde aliambatana na mgombea wa Kiti cha Makamu wa Rais kwa tiketi ya Chama hicho, Azza Haji Suleiman.




Comments
Post a Comment