MGOMBEA URAIS WA NLD DOYO HASSAN DOYO ACHUKUA FOMU INEC
Na Mwandishi wetu
MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele leo Agosti 10, 2025 amekabidhi fomu ya uteuzi kwa mgombea wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano kutoka Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo. Hafla hiyo imefanyika kwenye ofisi za Tume zilizopo Njedengwa Jijini Dodoma.
Doyo aliambatana na mgombea wa Kiti cha Makamu wa Rais kwa tiketi ya Chama hicho, Chausiku Khatib Mohamed.




Comments
Post a Comment