MGOMBEA URAIS WA UPDP TWALIB KADEGE ACHUKUA FOMU INEC
Na Mwandishi wetu
MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele leo Agosti,10, 2025 amekabidhi fomu ya uteuzi kwa jina la Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano kutoka Chama cha United Peoples' Democratic Party (UPDP), Twalib Ibrahim Kadege.
Hafla hiyo imefanyika kwenye ofisi za Tume zilizopo Njedengwa Jijini Dodoma.
Kadege aliambatana na Makamu wa Rais wa tiketi ya Chama hicho, Abdalla Mohamed Khamis.




Comments
Post a Comment