MTENDAJI MKUU WMA ATEMBELEA MAONESHO YA NANENANE DODOMA
Na Mwandishi wetu
OFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Alban Kihulla, leo Agosti 8, 2025 ametembelea Maonesho ya NaneNane kitaifa, uwanja wa Nzuguni jijini Dodoma.
Akiwa katika Banda la WMA, Afisa Mtendaji Mkuu amewapongeza watumishi wa Wakala kwa kazi nzuri ya kuelimisha umma ambao wamekuwa wakiifanya tangu kuanza kwa Maonesho hayo.
Amewataka kuendelea kutoa elimu kwa jamii hata baada ya Maonesho ili wananchi waelewe ni kwa namna gani kupitia WMA inawalinda Serikali kwa vipimo vinavyotumika katika sekta mbalimbali ni sahihi na vinatumika kwa matumizi.
"Tuendelee kutumia majukwaa mbalimbali kutoa elimu ya vipimo kwa wananchi ili waelewe haki yao ya kupata huduma kwa vipimo sahihi lakini pia na wajibu wao wa kushughulikia wanatumia vipimo sahihi katika sekta mbalimbali.
Kihulla ametembelea mabanda mengine likiwemo banda la Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Taasisi zake ili kujionea huduma zinazotolewa.


Comments
Post a Comment