MWAIJOJELE WA CCK ACHUKUA FOMU YA URAIS INEC
Na Mwandishi wetu
MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele leo Agosti 12, 2025 amekabidhi fomu ya uteuzi kwa mgombea wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano kutoka Chama cha Kijamii (CCK), David Daud Mwaijojele.
Hafla hiyo imefanyika kwenye ofisi za Tume zilizopo Njedengwa Jijini Dodoma.
Mwaijojele aliambatana na mgombea wa Kiti cha Makamu wa Rais kwa tiketi ya Chama hicho, Masoud Ali Abdala.





Comments
Post a Comment