REA YATOA ZAIDI YA BILIONI 4 KUZALISHA UMEME WA MAJI LUPALI



Utekelezaji wa mradi wa kufikia asilimia 98

Bodi ya nishati Vijijini yasisitiza mradi ukamilike kwa wakati

Mradio matumizi ya nishati rafiki na mazingira

Na Mwandishi wetu, NJOMBE 

WAKALA wa Nishati Vijijini (REA), imetoa kiasi cha shilingi bilioni 4.6 kwenye mradi wa kuingia umeme wa maji Lupali wenye uwezo wa kuzingatia kilowati 317 unaotekelezwa na shirika la Benedictine Sisters of St. Gertrud Convent Imiliwaha. 

Hayo yamebainishwa leo Agosti 1, 2025 na Mjumbe wa Bodi, Bw. James Mabula wakati. kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu, walipotembelea mradi wa Lupali unaotumia nguvu ya maporomoko madogo ya maji ya mto Lupali katika kuu umeme mkoani Njombe. 

Amesema kuwa, fedha zilizotolewa na REA zimewezesha ujenzi wa kituo cha msaada wa umeme na kituo cha msaada kwenye kituo cha Imiliwaha Sisters Convent pamoja na vijiji jirani vya Boimanda, Kitulila na Matola sambamba na kuwezesha tafiti za mradi huo.



"Hii ni pamoja na gharama za utafiti wa awali wa mradi, ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme (11kV) kilomita 23.48 na njia ndogo ya kusambazia umeme kwa kilomita 30. 6 Amesema Mabula. 

Aidha, utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 98 ambapo kazi utekelezaji hadi sasa ni pamoja na ujenzi wa kizuizi cha maji na mtaro wa kupitisha maji ya mafuriko ambao tayari umekamilika. 

Ameongeza, wamekamilisha ujenzi wa kituo cha nguvu cha umeme (Powerhouse, mfereji wa kurudisha maji mtoni pamoja na ujenzi bomba la kusafirisha vifaa na ununuzi wa vifaa vya umeme uliofikia asilimia 90.




Kwa upande wake, Mshauri wa Biashara wa mradi huo, Malimi Sitta amesema kuwa, mara baada ya mradi kukamilika, umezalisha utauzwa moja kwa TANESCO ambapo mkataba wa kuuzia umeme umeshasainiwa.

Ameongeza za mradi utakapokamilika utaongeza upatikanaji wa uhakika kwa wananchi kwa matumizi ya nyumbani na biashara na kupinguza matumizi ya nishati isiyo rafiki na mazingira. 

Ziara ya REB mkoani Njombe imelenga kutekeleza miradi ya REA inayotekelezwa katika huo sambamba na kupitia changamoto za waendelezaji wa miradi ya umeme huo hapa nchini na kupatiwa ufumbuzi.


Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA