SALUM OMARY: SITAWAANGUSHA WANANCHI WA PUGU STESHENI

 



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MGOMBEA udiwani wa Kata ya Pugu Stesheni kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Salum Shaibu Omary,  ameahidi kuwatumikia wananchi wa kata hiyo kwa moyo na uaminifu mkubwa.

Akizungumza Jijini Dar es salaam mapema leo Agosti 15,2025 mara baada ya kukabidhiwa barua ya uteuzi, katika Ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)Wilaya ya Ilala ,Salum amesema uteuzi huo ni ishara ya imani kubwa aliyopewa na CCM na kwamba hatowaangusha wananchi wa Pugu Stesheni.

“Nimefurahi kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi. Ninaahidi kwenda kuwatumikia wananchi wa Pugu Stesheni kwa moyo wangu wote na kwa kuzingatia ilani ya CCM,” amesema Salum.




“Kwa uwezo wa Mungu, nitawafanyia mambo makubwa na mazuri. Lengo langu ni kuona Pugu Stesheni inakuwa mfano wa kata bora ndani ya Manispaa ya Ilala,” amesisitiza.



Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA