TFS YANG’ARA SELOUS MARATHON, YATUMIA MICHEZO KUHAMASISHA UHIFADHI NA UTALII WA NDANI



Na Mwandishi Wetu, Morogoro

MASHINDANO ya Selous Marathon yaliyofanyika leo, Agosti 23, 2025 kwa mara ya saba mkoani Morogoro, yameendelea kuvutia maelfu ya washiriki na mashabiki. Miongoni mwa taasisi zilizong’ara ni Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), ambao wameonesha taswira mpya ya ushiriki wa kitaifa kwenye michezo kama nyenzo ya kukuza utalii na afya ya jamii.

TFS, ikiwa mmoja wa wadhamini wakuu wa mashindano, ilishiriki kupitia watumishi wake 35 waliokimbia kilomita 21, 10 na 5. Kupitia ushiriki huo, taasisi hiyo ilitumia mashindano haya kama darasa la vitendo kuendeleza dhana ya utalii wa michezo, kuhamasisha umuhimu wa uhifadhi wa misitu na kuongeza uelewa wa jamii kuhusu vivutio vya asili vilivyopo nchini.




Akizungumza baada ya kukimbia mbio za kilomita 10, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa TFS, Hussein Msuya, alisema ushiriki huo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya viongozi wa taasisi kuhakikisha michezo inakuwa sehemu ya maisha ya kila mfanyakazi ili kupambana na magonjwa yasiyoambukiza na kuimarisha utendaji.


“Ushiriki wetu Selous Marathon si kwa ajili ya mashindano pekee, bali ni kuthibitisha kwa vitendo dhana ya utalii wa michezo kama kaulimbiu yetu inavuosema "Kimbia ukitalii". Tumeimarisha afya za watumishi wetu, tumeeneza ujumbe wa uhifadhi, na tumechangia kukuza utalii wa ndani kupitia vivutio vya asili vilivyo chini ya usimamizi wa TFS,” alisema Msuya.



Aliongeza kuwa michezo imeendelea kuthibitisha nafasi yake katika kujenga taifa, akimnukuu Rais Samia Suluhu Hassan ambaye mara kadhaa amesisitiza umuhimu wa michezo kama sekta yenye mchango mkubwa kiuchumi, kijamii na kiafya.

Kwa upande wake, Ofisa Utalii wa TFS, Salome Kivuyo, alisema taasisi hiyo ilijitofautisha kwa washiriki wake kuvaa jezi maalum zilizoandikwa Visit Hululu Waterfalls, tofauti na zile zilizotolewa na waandaaji wa mashindano.

“Tulitumia mbio hizi kama jukwaa la kutangaza moja ya vivutio vyetu vikubwa Maporomoko ya Maji ya Hululu yaliyopo katika Msitu wa Mazingira 

Asilia Uluguru, ulio chini ya usimamizi wa TFS. Maporomoko haya ni kivutio cha kipekee chenye maji safi yanayotirika

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA