UZALISHAJI UMEME KWA KUTUMIA NISHATI JADIDIFU UMEFIKIA ASILIMIA 67- KAMISHNA LUOGA
Amshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi ya Nishati Jadidifu
Mafunzo ya mafunzo ya teknolojia ya Nishati ya Jua kwa wataalamu
Na Mwandishi wetu
TANZANIA imeendelea kuongeza vyanzo vya nishati kwa kutumia nishati jadidifu hadi asilimia 67, ikijumuisha matumizi ya nishati ya maji na Jua.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga wakati akifunga mafunzo ya wataalam kutoka taasisi mbalimbali zilizohusu usanifu, kuweka na ufungaji wa kanuni za Nishati ya Jua pamoja na matumizi yake.
Akifunga mafunzo hayo Mhandisi Luoga amesema mafunzo kuhusu nishati ya Jua yamefanyika nchini kwa sababu Tanzania imepiga hatua kubwa katika matumizi ya nishati na jadidifu.
Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya Nishati Jadidifu nchini.
Amesema washiriki kutoka katika taasisi mbalimbali wameshiriki mafunzo ya Nishati ya Jua yanayojulikana kama SOLTRAIN + ambayo yameandaliwa na Wizara ya Nishati kwa kitengo cha Kituo Mahiri cha Matumizi Bora ya Nishati na Nishati Jadidifu (SACREE) ambayo kipo chini ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizo Kusini mwa Afrika ( SADC).




Comments
Post a Comment