"WAHENGA”AAHIDI KUWATUMIKIA WANANCHI KATA YA KINYEREZI KWA MOYO MMOJA.




Na Mwandishi wetu

MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Kinyerezi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Ryoba Mrema, maarufu kama “Wahenga”, ameahidi kuwatumikia wananchi wa Kinyerezi kwa uadilifu, uwazi na moyo wa kujitolea ikiwa watampa ridhaa ya kuwaongoza katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

Mrema ameyabainisha hayo mapema leo Agosti 15,2025 mara baada ya kukabidhiwa barua ya uteuzi kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Chief Sylvester Yared, Mrema amesema uteuzi huo ni heshima kubwa na kwa familia yake, huku akiahidi ufadhili za maendeleo katika kata hiyo.




“Sisi familia yetu ni watu wa kawaida kabisa, lakini nimeaminiwa na wajumbe. Chama kimeniamini, na sasa nimepata nafasi ya kuomba ridhaa kwa wananchi wa Kata ya Kinyerezi ili wanichague kuwa diwani wao. Lengo ni gurudumu la maendeleo kwa karibu wa karibu,” amesema Mrema.

Aidha, amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira ya ushindani wa haki ndani ya chama na kutoa nafasi kwa kila mwenye nia njema ya kuwatumikia wananchi.



Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA