WIZARA YA NISHATI YAJIVUNIA UTEKELEZAJI WA MIRADI SABA KATI YA 17 NCHINI

 



Katibu Mkuu Nishati asema kati ya miradi hiyo saba, JNHPP imekamilika
Asema EACOP imefikia asilimia 65 huku Serikali ya Tanzania ikichangia hisa za shilingi trilioni 1.12

Ruhudji na Rumakali tafiti zakamilika

Na Mwandishi wetu

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba amesema kuwa katika miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Wizara ya Nishati inatekeleza takriban miradi saba.

Mhandisi Mramba ameyasema hayo Agosti 17, 2025 wakati wa kitengo cha Mpango wa Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa Vijana (YEE) ambao unagusa maeneo yanayopitiwa na mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).

“Miradi hiyo ni mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), Mradi wa kugeuza gesi kuwa kimiminika (LNG), Mradi wa utafutaji, Miradi ya umeme ya Rumakali na Ruhudji na utafiti wa mafuta eneo la Mnazi Bay North”, amesema Mramba.




Ameeleza kuwa katika miradi hiyo saba, mradi wa kuamsha umeme kwa maji ya Julius Nyerere unaozalisha megawati 2,115 umekamilika na unaingiza umeme kwenye gridi ya Taifa.

Ameongeza kuwa mradi wa bomba la mafuta ghafi (EACOP) umefikia asilimia 65 na upo mbioni kukamilika, mradi wa LNG upo katika hatua za mwisho na miradi ya umeme ya Ruhudji na Rumakali tafiti zimekamilika.

Aidha, amesema Serikali ya Tanzania imeshachangia takribani shilingi trilioni 1.12 kwenye mradi wa EACOP kama hisa ya Tanzania katika mradi huo na kuna kampuni ya kitanzania 200 ambazo zinatekeleza kazi mbalimbali katika mradi wa EACOP ambazo zitalipwa jumla ya shilingi trilioni 1.325.


Mhandisi Mramba ametanabaisha kuwa na fursa za fursa zinazopatikana pia maeneo katika maeneo ambayo umeme unaopeleka umeme EACOP itapita watanufaika kwa kuunganisha na huduma ya umeme.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA