BOT, BENKI KUU YA RWANDA KUSHIRIKIANA KUBORESHA SEKTA YA FEDHA



Na Mwandishi wetu

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Emmanuel Tutuba, amesema Benki Kuu ya Tanzania itaendelea na Benki Kuu ya Rwanda (NBR) kubadilishana uzoefu kwenye maeneo mbalimbali ya kustawisha sekta ya fedha na uchumi wa nchi zote mbili.

Gavana Tutuba ameyasema hayo alipokutana na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Jenerali Patrick Nyamvumba, ambaye alitembelea ofisi za Benki Kuu jijini Dar es Salaam , tarehe 9, Septemba, 2025.

Akizungumza katika kikao hicho, Balozi Jenerali Nyamvumba aliipongeza Benki Kuu kwa kuwa na ubunifu unaoleta mageuzi katika sekta ya fedha nchini hususan katika masuala ya malipo ambayo inarahisisha ufanyaji biashara nchini humo pamoja na mpango wa Benki Kuu wa ununuzi wa dhahabu. 


Alisema kuwa Benki Kuu ya Rwanda inajifunza jinsi BOT inavyotumika malipo ya taifa na kutekeleza mpango wa ununuzi wa dhahabu kwa ajili ya kutunisha fedha za kigeni.

Kwa upande wake Gavana , Emmanuel Tutuba alimueleza Balozi huyo kuwa Benki Kuu ya Tanzania kupitia wataalam wake wa ndani imetengeneza Mfumo wa Malipo wa Papo kwa Hapo (TIPS) ambao umeleta mageuzi makubwa na unafuu wa kufanya malipo kwa njia ya kielektroniki nchini. 




Aliongeza uhusiano wa kibiashara kati ya nchi mbili unaleta chachuongeza kufanya hivi kuboresha mbinu ya malipo ili kurahisisha na kuongeza idadi na kiasi cha miamala inayofanyika kati ya Tanzania na Rwanda.

Kuhusu mpango wa ununuzi wa dhahabu Gavana alisema kuwa tangu tarehe 1 Oktoba 2024 Benki Kuu ilipoanza rasmi ununuzi wa dhahabu hadi Agosti 2025, jumla ya tani 9.165 za dhahabu zenye thamani ya takribani Dola za Marekani milioni 1,015.98 zimekwisha kununuliwa.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA