DOYO AGUSIA MKONGE KAMA URITHI WA TANGANYIKA, AHIDI KUREJESHA THAMANI YAKE
Na Mwandishi Wetu
MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo, akiwa Korogwe amezungumzia zao la mkonge na kulihusisha na historia ya taifa tangu enzi za ukoloni, ambapo Tanga ilijulikana kimataifa kama kitovu cha zana za mkonge.
Hata hivyo, amesema kwa miongo mingi wakulima wa mkonge wamekumbwa na changamoto za soko, teknolojia duni na sekta ya viwanda kuchakata kwa kiwango cha kisasa, hali iliyowalazimu kuishi kwa imani badala ya kunufaika na jasho lao.
Katika kampeni zake wilayani Korogwe, Doyo aliibua upya mjadala kuhusu thamani ya zao, akiahidi kujenga kiwanda cha kuchakata mkonge hilo na wakulima wanapatiwa pembejeo bure. "Mkonge unaweza kututoa kwenye umasikini. Tatizo limekuwa katika teknolojia ya teknolojia na ukosefu wa dhamira ya kisiasa. Nikipata ridhaa ya kuwa Rais, nitahakikisha tunaongeza thamani ya zao hili kwa manufaa ya wananchi," alisema Doyo.
Wataalamu wa kilimo wanasema mkonge una nafasi kubwa katika viwanda vya nguo, kamba, na bidhaa nyinginezo zinazohitajika kulipwa. Wakati mataifa ya Amerika na Asia yamewekeza katika teknolojia za kisasa, Tanzania bado imeendelea kutumia mbinu zinazopunguza ubora wa zao hilo.
Aidha, Doyo alisema iwapo wananchi wa Korogwe na maeneo mengine watamchagua, atahakikisha kiwanda kipya kitawanufaisha wakulima kwa kuwawezesha kuuza bidhaa zilizoongezwa thamani badala ya malighafi ghafi pekee. Hatua hiyo, alisema, itaongeza kipato cha wakulima na kutafuta ajira mpya kwa vijana na wanawake nchini. “Kwa miaka mingi, wakulima wa Korogwelalamikia mikopo yenye masharti magumu na pembejeo isiyo na ubora.
Ahadi hizo zimepokelewa kwa shangwe na wananchi wa Korogwe, hususan wanawake ambao mara nyingi wamekuwa wahanga wa mikopo kandamizi.
Kampeni za NLD zinaendelea, huku msafara wa mgombea huyo wa urais ukielekea Lushoto, Handeni, Kilindi na hatimaye Kiteto.



Comments
Post a Comment