ILANI YA NLD ITALETA SULUHISO KAMILI KUHUSU AJIRA, UTAFITI NA TEKNOLOJIA DOYO.




Na Mwandishi wetu,SIMIYU


MGOMBEA urais kupitia Chama cha NLD na Katibu Mkuu wa chama hicho, Hassan Doyo, akiendelea na kampeni zake mkoani Simiyu, amewaambia wananchi kuwa moja ya changamoto zinazokwamisha maendeleo ya Tanzania ni mfumo wa elimu na usiokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na mahitaji ya taifa.


Akihutubia mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Lamadi, Wilaya ya Busega, Doyo kuwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 64 ya uhuru, elimu ya Tanzania imeendelea kujikita zaidi katika nadharia na vijana, hali inayosababisha wengine kukosa ujuzi wa vitendo unaowawezesha kuajiriwa au kujiajiri.


“Kwa mfano, nchini China, mtoto mwenye umri wa miaka minne hadi kumi tayari hupatiwa elimu inayojikita kwenye stadi na ujuzi wa vitendo. Hivyo vijana hao wanakua wakiwa na uwezo wa kuchangia katika maendeleo ya taifa wakiwa bado wadogo. Hali hii Tanzania bado hatujaifikia,” alisema  Doyo.


Doyo kuwa, kwa mujibu wa ilani ya uchaguzi wa NLD, chama hicho kimejipanga kufanya kazi kubwa ya elimu ili kuhakikisha kila mtoto anayemaliza masomo anakuwa na ujuzi unaomuwezesha kuishi kwa uwezo. Mpango huo unajumuisha vituo vya utafiti na teknolojia katika kila kanda na halmashauri nchini, ili kuwapa vijana nafasi ya kubuni, teknolojia mpya, na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Serikali inapohitajika.


“Tunataka elimu itakayokuwa suluhisho la moja kwa moja kwa tatizo la ajira. Vijana wakiwezeshwa kupitia elimu ya ufundi na teknolojia, hawatakuwa na elimu tena. Hatutaki kuona mzazi kuuza mtoto kumsomesha, halafu mtoto huyo akimaliza shule anarudi nyumbani na kuendelea kumtegemea mzazi yuleyule. Elimu hiyo sisi NLD tunakwenda kuiondoa kabisa Tanzania,” alisisitiza Mhe. Doyo.


Aidha, Doyo alisema kuwa ilani ya Chama cha NLD imeeleza kwamba mageuzi hayo ya elimu yatafungamanishwa na vyuo vikuu vya ufundi, teknolojia na ubunifu, ili kuondoa changamoto ya vijana kupata sababu ya ukosefu wa uzoefu.


“Leo vijana wakitaka ajira wanaambiwa lazima uwe na uzoefu wa miaka mitatu ili waweze. Sisi tunasema hapana. Elimu yenye ubora na uzoefu wa kweli wa mwanafunzi. Kupitia mfumo mpya, kila kijana atakuwa na ujuzi wa moja kwa moja wa kuingia kwenye soko la ajira au mradi wake binafsi,” alisema.


Kwa mujibu wa hayo, sera za NLD zinalenga kujenga kizazi cha Watanzania chenye uwezo wa ubunifu, bilategemea ajira za serikali pekee, na kinachochangia katika uchumi wa taifa kwa haraka.


Msafara wa urais huyo wa NLD upo Simiyu katika muendelezo wa kumnadi wa Chama hicho Mhe. Doyo Hassan Doyo .

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA