KAMPUNI YA VIOO DAR ES SALAAM YAJIVUNIA MIAKA 45 YA UBORA NA UZOEFU SEKTA YA UJENZI.



Na Mwandishi wetu

KAMPUNI ya Dar es Salaam Class Warks inayojishughulisha na kazi za usimikaji wa vioo kwa majengo mbalimbali imeeleza mafanikio yake makubwa katika kipindi cha zaidi ya miaka 45 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1989, huku ikijivunia kushiriki kwenye miradi mikubwa ya Serikali, biashara na watu binafsi.

Akizungumza na waandishi wa habari  Meneja wa Masoko  wa kampuni hiyo, Hassanali Talib katika kongamano la umoja wa wakandarasi na watoa huduma Shirikisho Tanzania (TUCASA).

Amesema kuwa kampuni hiyo ilikuwa ya kwanza kuanzisha huduma ya usimikaji wa vioo nchini Tanzania na imeendelea kuwa kinara katika ubunifu, ubora na usalama wa kazi zake.

“Mojawapo ya mafanikio makubwa ni kushiriki katika mradi wa ujenzi wa Mji Mpya wa Serikali Mtumba, Dodoma, ambapo tumeweza kusimikwa vioo katika majengo ya wizara zaidi ya 11. Hii ni heshima kubwa kwetu kama kampuni ya kizalendo,” amesema 



Ameongeza kuwa, kwa upande wa majengo binafsi, kampuni imekuwa ikihudumia wateja katika maeneo mbalimbali kwa kutumia teknolojia za kisasa na vioo vyenye ubora wa hali ya juu ili kuhakikisha usalama wa majengo na watumiaji wake.

“Tunatumia vioo vinavyokidhi viwango vya kimataifa, tukizingatia usalama wa jengo na watanzania kwa ujumla. Hili ni jambo tunalolipa kipaumbele katika kila mradi tunaufanya,” alisisitiza.



Aidha, aliwataka watanzania kufika katika ofisi za kampuni hiyo ili kupata elimu kuhusu matumizi bora ya vioo kwenye ujenzi wa kisasa, huku akibainisha kuwa kampuni hiyo ina wataalam waliobobea katika sekta hiyo na wenye uzoefu wa kutosha.


Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA