MASANJA MKANDAMIZAJI ATANGAZWA BALOZI WA MWANGAZA STATIONERY & SUPPLY

 


Awahimiza watanzania kununua vifaa vya kisasa vya ofisini

Na Mwandishi wetu

MTUMISHI wa Mungu na msanii maarufu nchini, Emmanuel Mgaya Masanja Mkandamizaji, ametangazwa rasmi kuwa Balozi wa Kampuni maarufu Stationery & Supply, hatua inayolenga kuwaelimisha kuhusu Watanzania matumizi ya vifaa, vya kisasa vinavyokidhi mahitaji ya kiteknolojia katika ofisi na taasisi mbalimbali.

Akizugumza Jijini Dar es salaam mara baada ya uteuzi huo, Masanja amesema ameamua na Kampuni ya Mwangaza kutokana na ubora wa bidhaa zinazotolewa na kampuni hiyo, kupitia vijana wenye ujuzi na weledi mkubwa sekta ya vifaa vya ofisini.

 “Kiukweli, kupitia Mwangaza, kile kilio cha watu wanaohitaji vifaa vya ofisini ubora wa hali ya juu kitapatiwa suluhisho. Zao vina viwango vya kimataifa na vinapatikana kwa bei nafuu,” amesema Masanja.




Aidha, kampuni imesema kuwa kampuni hiyo ni chanzo cha bidhaa, bali ni msaada halisi kwa taasisi, kampuni na wananchi wanaohitaji vifaa vya kisasa vya ofisini.

 “Mwangaza si tu jina la kampuni, bali ni mwanga halisi kwa wale wanaotafuta bidhaa bora, huduma ya haraka, na gharama rafiki,” amesisitiza. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mwangaza Stationery & Supply, Eunice Bushanga amesema kampuni hiyo imefurahishwa na huo na ina imani kuwa na umaarufu na ushawishi wa Masanja, Watanzania wengi zaidi wataweza kufahamu na kupata bidhaa zao kwa urahisi.



"Tunayo furaha kubwa kumkaribisha Masanja Mkandamizaji kama balozi wetu. Tunaamini huu utaleta mwanga zaidi kwa Watanzania katika kuchagua vifaa bora vya ofisini," amesema Eunice. 


Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA