MATENGENEZO MTAMBO WA RUVU JUU YAKAMILIKA





Na Mwandishi wetu

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imekamilisha matengenezo ya dharura ya Saa 18 dharura katika Mtambo wa kusukuma maji Ruvu Juu uliopo Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani yaliyopelekea kupungua kwa huduma ya maji kwa wakazi wanaohudumiwa wa Mlandizi hadi Kisarawe.

Akizungumzia kukamilika kwa kazi hiyo, Meneja wa Mtambo wa Ruvu Juu mhandisi Juma Kasekwa amesema kazi imefanyika mchana na usiku ili kukamilisha matengenezo haya muhimu.


"Matengenezo haya ya dharura yalitokana na changamoto katika pampu zetu za kusukuma maji, kazi ya matengenezo ilianza jana, Septemba 22,2025 na yamedumu kwa saa 16. Kwasasa matengenezo yamekamilika na pampu zinaendelea kusukuma maji katika kawaida yake" ameeleza Mhandisi Kasekwa 



Kukamilika kwa matengenezo haya kutaboresha huduma ya maji kwa wakazi wa Mlandizi hadi Kisarawe katika maneno ya Chalinze, Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mabwawa, Visiga, Maili 35, Maili Moja, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mbezi Kimara, Tabata Segerea, Kinyerezi, Kisukuru, Saranga, Bonyokwa, Msigani, Maramba Mawili, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA