MBETO: AMANI NA UMOJA FUNGUO ZA MILANGO YA MAENDELEO
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM )kimesema hakitaacha kuzihimiza Serikali zake zizidishe mkazo na kulinda hakuna mtu au kikundi chochote kinachoweza kuvuruga Amani na Umoja.
Vile vile chama hicho kimefichua siri ya mbele kwa maendeleo ya haraka katika Awamu ya Nane Zanzibar ni kuwepo kwa Ustawi wa Amani na Utulivu .
Hayo yamebainishwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo, Khamisi Mbeto Khamis, aliyesema nchi ikiwa katika mazingira ya Umoja ,milango ya neema ya Maendeleo hufunguka.
Mbeto alisema inapokosekana Amani , Mshikamano na Utulivu , Serikali haiwezi kujenga miradi mikubwa kama ya Madaraja, Maji, Shule, Barabara, Bandari, Viwanja vya Ndege , Michezo na Masoko.
Alisema kwa muktadha huo , CCM imekuwa ikizielekeza mara zote Serikali zake zihakikishe hachekewi mtu yeyote atakaethubutu kuvuruga tunu za Amani na Umoja wa Kitaifa .
Pia Mbeto alitaja kufanikiwa kwa ujenzi wa miradi ya maendeleo, kuchochewa zaidi na kasi ya kutafuta Mapato kwa umakini kuliko kujenga miradi yenye nguvu.
"Serikali ya CCM Awamu ya Nane Zanzibar imejitahidi mno kukusanya .Si hivyo tu lakini pia imesimamia nidhamu ya matumizi ya fedha. SMZ sasa inakopesheka mahali kuliko wakati wowote "Alieleza
Hata katika maelezo yake Mbeto alisema SMZ hivi sasa ina kibali cha kutoa wa kukopa katika taasisi za fedha kwenye benki zote.
'Tunaingia kwenye mbio za Uchaguzi huu tukiwa na mategemeo makubwa ya kushinda.Mgombea wetu Rais Dk Mwinyi ni kiongizi mchapakazi , muaminifu na mzalendo "Alisema .
Katibu huyo Mwenezi aliwahakikishia wananchi kuwa ushindi utakaopatikana katika ngwe ya, utazidi kutanua wigo wa maendeleo yatakayowashangaza wengi Afrika Mashariki .

Comments
Post a Comment