MBIO ZA KUKINADI CHAMA CHA MAPINDUZI MKOANI GEITA ZAANZA KWA KISHINDO, MAJIMBO 7 KATI YA 9 YAPITA BILA KUPIGWA



Kata 92 kati ya 122 zapita bila kupingwa

Maelfu wakusanyika kusikiliza Ilani ya CCM 2025-2030

Dkt. Biteko awasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kumpigia kura Dkt. Samia Suluhu Hassan

Asisitiza mshikamano kabla na baada ya uchaguzi

Na Mwandishi Wetu, Geita

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoani Geita leo Septemba 2, 2025 kimezindua kwa kishindo kampeni za kuinadi Ilani ya CCM 2025-2030 kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ambapo imeelezwa kuwa mpaka sasa tayari Majimbo 7 kati ya 9 ya Ubunge yamepita bila kupingwa huku kata 92 kati ya 122 zikipita bila kupingwa.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo uliofanyika katika Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe, Mkoani Geita ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa huo, Nicholaus Kasendamila amesema Chama cha Mapinduzi kinaingia kwenye kampeni kikiwa na mtaji mkubwa wa uadilifu, uaminifu, uchapakazi na busara ya mgombea Urais wa kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema kupitia kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, CCM inazo sababu za kuomba ridhaa ya wananchi kuendelea kuongoza nchi akisema kuwa amefanya maendeleo mengi ikiwemo uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam ambayo ni lango kubwa la biashara kwaTanzania na nchi jirani, amejenga daraja refu la Busisi, amekamilisha ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere (MW 2,115) na reli ya kisasa imeshaanza kufanya kazi.




Kasendamila amesema kuwa katika Mkoa wa Geita, Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025 imetekelezwa kwa mafanikio ambapo ameeleza kuwa shule mpya za msingi 151 zimejengwa, Shule za sekondari mpya 118 zimejengwa, zimejengwa hospitali mbili za rufaa, hospitali za wilaya mpya 4 na vituo vya afya 17 vipya vimejengwa.

Ameongeza kuwa, kupitia Ilani ya CCM 2020-2025, zahanati 69 zimejengwa, leseni za madini 7600 zimetolewa kwa wachimbaji wadogo na kuhusu umeme, kabla ya kuingia kwa Serikali ya Awamu ya Sita kulikuwa na vijiji 362 tu vyenye umeme lakini sasa vijiji vyote 486 mkoani Geita vina umeme.




Kuhusu miundombinu ya Barabara amesema Barabara za lami na changarawe zimeendelea kujengwa mkoani Geita ili kurahisisha usafiri wa wananchi. 

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA