MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBAGALA AFUNGUKIA ILANI YA CCM AWAHAKIKISHI USHIRIKIANO WALIMU


  


Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM 

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Mbagala Kakulu Burchad  amesema kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka huu kimetoa ahadi mbalimbali na katika sekta ya miundombinu ,elimu ,afya ,na katika maeneo yanayohusu kuendelea juzi.

Amesema kwa ufupi kwa eneo la mbagala Serikali inakusudia kutekeleza na kutatua changamoto za miundombinu ya Barabara zilizopo kupitia utaratibu wa kuboresha mji wa Dar es salaam DMDP2  na katika ilani ya CCM imetamka wazi kuwa eneo la mbagala watapanua Barabara kutoka rangi tatu kwenda Mwandege njia nne.

Mgombea huyo ubunge Kakulu ameyasema hayo Septemba 24 2025 kwenye hafla fupi ya mahafali ya kumaliza elimu ya msingi wanafunzi wa shule ya msingi mbagala  kuu ambapo  yeye alikuwa mgeni rasmi 


Kakulu amefafanua kuwa Barabara hiyo ya rangitatu mwandege njia nne itakuwa na mwendo Kasi lakini jambo lingine wanaendelea kupanua Hospitali ya Zakhem katika Sekta ya afya ambapo wanajenga jengo kubwa la gorofa sita na wanakusudia kitapunguza mzigo katika hospital ya rufaa temeke .

Amesema wakati wanazindua kampeni pale kawe mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi CCM DKT Samia Suluhu Hassan alitamka katika siku 100 za Kwanza atatoa Ajira 5000 Sekta ya afya ,na ajira 7000 Sekta ya elimu kwa maana walimu.

Ameongeza kuwa maeneo mengine ambayo yalipewa kipaumbele ni pamoja na kuhakikisha shule zinaweza kuchukua wanafunzi wakutosha,kuongeza madarasa , walimu,  hivyo yapo mengi  ila Ilani imejieleza 




Amesema pia  Serikali ya CCM imejipanga vizuri kuhakikisha eneo linalohusu kuongeza maalifa na kuhudumia Sekta ya elimu vizuri zaidi na katika siku mia Moja hizo hizo serikali inakusudia kujenga programu maalumu itakayohusu  kujenga vijana kwa kushirikiana na veta ili kuwapa uwezo zaidi hasa wa kujiari.

Naye Mwalimu mkuu wa shule ya msingi mbagala kuu Juliana lubuva amesema  wanafunzi  538  wamehitimu darasa la saba katika shule ya  Msingi Mbagala Kuu na kufanya mahafali  ya kuhitimu elimu ya msingi 

Amesema kwamba shule hiyo ilianza mwaka 1975 na darasa la saba kwa mwaka huu wa 2025 walikua wanafunzi 540 kati yao  wanafunzi 538 wamefanya mitihani na huku wengine wawili wakiwa hawajafanya mitihani kutokana na sababu mbalimbli na mmoja alikua mgonjwa

Mwalimu lubuva  amesema kwamba tangu mwaka 2021 Shule hiyo imekuwa ikipokea wanafunzi wengi lakini pia anaishukuru Manispaa ya Temeke,Afisa Elimu,Mkurugenzi na viongozi wote kwa ajili ya kuiwezesha shule hiyo  kwa kuwapatia madawati,majengo mengi yanatosheleza kwa wanafunzi.

Pia  amesema kwa upande wa taaluma shule imekuwa ikifanya vizuri kwa wanafunzi na ufaulu unaongezeka kila Leo kutokana na  walimu kuwa msitari wa mbele na wanafanya kazi kwa uadilifu mkubwa.

"Tunawashukuru wazazi wa wanafunzi wa shule hii Kwanza wamekua msaada mkubwa kwa shule kwani wanatusaidia kwa karibu na tunashirikiana nao vizuri ",amesema Mwalimu Mkuu Lubuva

Sanjari na hayo,amesema kwamba matarajio kwa mwaka huu "Tunaamini wanafunzi wote 538 wataendelea na masomo ya elimu ya sekondari."amesema 

Akimzungumzia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kiongozi huyo anatosha kuendelea kuwa kiongozi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani anafanya kazi kubwa na zinaonekana kwa macho.

Lubuva amewaomba wazazi na wananchi kwa ujumla kumpa kura za ndio na kuwachagua wabunge na madiwani ili waweze kushirikiana nao katika kuhakikisha wanafunzi wanapata haki yao ya kielimu na kutimiwa mahitaji muhimu hasa miundombinu mbalimbali yanayo changia kuboresha  taaluma.

Naye Mwanafunzi  Rufudati  Alhaj Buruhan  aliyehitimu Darasa la Saba shuleya msingi mbagala kuu amesema mategemeo yake ni kufaulu na darasani alikuwa anafanya vizuri masomo ya Uraia , Hesabati , Sayansi  na anapendelea kuwa mwanajeshi.

Pia amewashukuru walimu kwa kuweza kumlea vizuri na ameletwa shuleni hapo akiwa mdogo hadi sasa na wazazi wake anawashukuru sana kwa kumlea vizuri.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA