NLD YAHITIMISHA KAMPENI MIKOA YA KANDA KASKAZINI
Na Mwandishi wetu
CHAMA cha NLD kimehitimisha awamu ya kampeni katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini ikiwemo Tanga, Babati na Arusha.
Katika mikoa hii, chama kimefanikiwa kufanya zaidi ya mikutano 45 ya kampeni kwa mfumo wa kijiji kwa kijiji na kata kwa kata.
Mikutano hii imefanyika kwa mtindo wa mobile kampeni, ambapo Mgombea Urais amekuwa akiwafuata wananchi mahali walipo, huku timu ya kampeni ikiendelea na kampeni za nyumba kwa nyumba katika maeneo yaliyosalia mara baada ya mgombea kuhamia wilaya nyingine.
Mgombea Urais wa NLD amefika katika maeneo ya pembezoni kama vile, Jasini,Mkinga, Msomela, Handeni, na Mlalo, Lushoto, hiyo ni tofauti na wagombea wengine waliobaki mijini. Tathmini zinaonyesha kuwa wananchi wengi barani Afrika wanapenda kuthaminiwa, kujaliwa na kufuatwa kwenye makazi yao. Hali hii ya kuwafuata wananchi katika vijiji vyao inawapa nafasi kubwa ya kumsikiliza kwa makini mgombea wetu, na si tu kumsikiliza bali pia kumuelewa vyema kupitia sera na ilani ya chama chetu.
Kupitia mkakati huu wa kampeni shirikishi na ya ukaribu na wananchi, NLD imejipambanua kama chama kinachojali kada zote za wananchi na kinachothamini kila sauti ya kila Mtanzania, bila kujali umbali wa eneo husika. Tathmini zinaonyesha kuwa kati ya wagombea 16 wa Urais, Mhe. Doyo kupitia Chama cha NLD ni miongoni mwa wagombea wachache walioweza kuwafikia wananchi moja kwa moja katika vijiji vyao.
Baada ya mafanikio haya ya Kaskazini, NLD sasa inatarajia kuelekeza nguvu zake Kanda ya Ziwa, katika mikoa ya Mara, Mwanza, Geita, Bukoba na maeneo mengine, kwa lengo la kuendelea kuwa karibu na wananchi na kusikiliza changamoto zao moja kwa moja kwa mtindo wa mobile kampeni.

Comments
Post a Comment