RAIS MWINYI: UBUNIFU WA MAJENGO NI NGUZO MUHIMU KATIKA UCHUMI





Na Mwandishi wetu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema fani ya ubunifu wa majengo ni miongoni mwa sekta muhimu zinazochangia uchumi unaokua kwa kasi kila siku.

Dkt. Mwinyi aliyasema hayo tarehe 8 Septemba 2025, Ikulu Zanzibar, alipokutana na timu ya wabunifu wa majengo kutoka Taasisi ya Ubunifu wa Majengo ya Afrika Mashariki, wakiongozwa na Rais wa Taasisi hiyo, Mhandisi Mecky Tchawi.

Rais Dkt. Mwinyi aliihakikishia timu hiyo kuwa Zanzibar nimeanza kuchukua hatua za kitivu cha taaluma ya ubunifu wa majengo katika vyuo vikuu na taasisi za elimu juu, kutokana na umuhimu wake katika ukuaji wa uchumi na miradi ya ujenzi katika sekta mbalimbali za maendeleo. Aidha, alibainisha kuwa Serikali, kwa taasisi na taasisi hiyo, itatafuta mbinu za utekelezaji wa wazo hilo.



Katika mazungumzo hayo, Rais Dkt. Mwinyi pia ameridhia ombi la taasisi hiyo la kuwa mlezi wa kwanza mzawa wa Afrika Mashariki tangu kuanzishwa kwake 1913, na kukabidhiwa cheti maalum pamoja na kitabu cha historia ya taasisi hiyo.

Kwa upande wake, Rais wa Taasisi, Mhandisi Mecky Tchawi, kasi ya ujenzi wa majengo katika nchi yoyote katika kilelezo cha ukuaji wa uchumi wake. Alisisitiza kuwa Zanzibar ni kuwa na kitivu cha taaluma ya ubunifu wa majengo ili kuandaa wabunifu vijana wenye ujuzi na weledi wa kisasa.





Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA