REA YAUZA MAJIKO 1500 KWA BEI YA RUZUKU KWeNYE MAONESHO YA MADINI GEITA
REA yapongezwa kwa kuuza majiko kwa bei ya ruzuku na kutoa elimu ya miradi ya wakala
Na Mwandishi wetu, GEITA
MAONESHO ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita yamehitimishwa rasmi na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ambayo yalifunguliwa Septemba 18 na kufikiria kilele tarehe 28 Septemba, 2025
Wakala umeshiriki maonesho hayo kwa kutoa elimu ya nishati safi ya kutuma, kutoa elimu ya miradi inayotekelezwa na wakala wa vijijini pamoja na fursa zinazopatikana kwa wakala kama vituo vya mafuta.
Sambamba na hayo Wakala unahamasisha matumizi ya kuuza kwa kuuza kwa ruzuku ya gesi ya kilo 6 ambayo inauzwa kwa bei ya 50% ambayo ni kiasi cha shilingi 17,500 ambapo jumla ya mitungi 5,00 imeuzwa kwa ruzuku kwenye maonesho.
Pamoja na hayo, Wakala unafadhili uuzwaji wa majiko banifu yanayotumia mkaa mbadala pamoja na mkaa wa kawaida, majiko hayo yameuzwa kwa bei ya ruzuku ya 85% ambayo ni shilingi 6,195 ambapo bei yake ya kawaida ni shilingi 41,300 ambapo majiko banifu 1,000 yatauzwa kwa bei ya ruzuku katika maonesho hayo.
Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini 2025 yamefanyika katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili mkoani Geita.



Comments
Post a Comment