RIDHIWANI KIKWETE AZINDUA KAMPENI KWA KISHINDO CHALINZE, AHIDI MAKUBWA

 


Na Mwandishi wetu 

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Chalinze Wilaya ya Bagamoyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete jana September 15, 2025 amezindua rasmi kampeni zake za Ubunge zilizofanyika uwanja wa Mdaula ambapo ameahidi kufanya makubwa ikiwemo utekelezaji wa Maji na Miundombinu.

Awali mgeni rasmi katika kampeni hizo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani Zainabu Vullu ameweza kuwashukuru Wananchi wa Jimbo hilo kwa kujitokeza kwa wingi na amemuombea kura Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  huku akimuelezea kama Mwanadiplomasia mahiri duniani na ameahidi akichaguliwa kupitia ilani ya 2025-2030 atahakikisha anaboresha huduma za afya, elimu, miundombinu.

Aidha, Zainabu Vullu amemuelezea Ridhiwani Kikwete ni mchapakazi na mwenye uthubutu na kuwataka Wananchi wa Chalinze kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 kumpa kura nyingi za Ndiyo, Mbunge Ridhiwan na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Madiwani wote wa CCM.




Nae  Ridhiwani Kikwete amewashukuru wana Chalinze kwa namna ya kipekee ambapo amewahidi kukamilisha mambo mbalimbali katika kuendelea kuwatumikia hasa huduma ya maji kwa asilimia 100.

Ambapo amesema huduma ya maji itazifikia Kaya zaidi ya 300,000 kutoka kaya zaidi ya 90,000 kwa miaka mitano iliyopita ambapo maji yanapatikana kwa asilimia 92.

"Nikichaguliwa nitakabiliana na moja ya changamoto ya upatikanaji wa maji kwa kuwafikishia wananchi majumbani badala ya vioski na kuzifikia kaya hizo 300,000," amesema Ridhiwani Kikwete.

"Kwa upande wa miundombinu tutanunua greda kwa ajili ya kuchonga barabara na kujenga vituo vinne vya mabasi, ujenzi wa hoteli ya kisasa yenye hadhi ya nyota nne ambayo itakuwa na ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kuongeza mapato," amesema Ridhiwani Kikwete.




Katika tukio hilo la uzinduzi,  Ridhiwani Kikwete ameweza pia kutangaza kikosi kazi cha kampeni zake ndani ya Jimbo, ikiwemo Kampeni Meneja wake, Mariamu Mkali, Halima Dossa na Haji Mgeni ambao watapita katika Jimbo hilo kuomba kura za ushindi kwa Mbunge, Rais na Madiwani.

Kwa upande wake Mratibu wa kampeni kanda ya Pwani Richard Kasesela amesema kuwa watu waliojiandikisha wahakikishe wanajitokeza kuwapigia kuwa wagombea wa CCM.



Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bagamoyo Abubakar Mlawa amesema kuwa chama kimejipanga kuhakikisha Rais anapata kura za kishindo sambamba na Wabunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete na Bagamoyo Subira Mgalu na Madiwani wa Kata 15 za Chalinze.



Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA