SERIKALI YA AUSTRIA KUFADHILI MIRADI YA UMEME TANZANIA
Ni inayozalisha umeme kutokana na Jua Takataka
Ufadhili huo ni kupitia Benki ya UniCredit ya Austria
Serikali ya Tanzania yaahidi
Na Mwandishi wetu
SERIKALI ya Austria kupitia Benki ya UniCredi imeahidi kuipatia fedha Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kiasi cha Euro Milioni 20 sawa na takribani Shilingi bilioni 60 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kumaliza umeme kwa kutumia jua na takataka.
Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Merl Solar Technologies GmbH, Hannnes Merl alipofanya mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba Septemba 17, 2025 pembeni ya Mkutano Mkuu wa 69 wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomic unaoendelea Jijini Vienna, Austria.
Mhandisi Mramba ameikaribisha kampuni hiyo nchini Tanzania ili kukutana na kufanya kazi kwa bidii katika miradi hiyo mipya ya umeme huku akiahidi kutoa umuhimu wa kutekeleza miradi hiyo.
Felchesmi Mramba ameeleza kuwa kampuni ya Merl imeshatekeleza miradi mbalimbali ya umeme wa jua nchini akisema “kampuni hii imetekeleza miradi ya umeme katika vijiji kumi (10) katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2017”.
Ametaja miradi hiyo kuwa ni ya makontena 14 ya umeme kwa kutumia nishati ya jua katika Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Mlele mkoani Katavi, pamoja na Uyui mkoani Tabora ambapo mradi huo uligharimu kiasi cha shilingi 16.2.
Ameongeza kuwa miradi hiyo imewezdsha kuzipatia umeme nyumba na makazi 812, nyumba za Ibada 27, Shule 6 na Vituo vya Afya 8.
Mramba ameiambia Serikali ya Austria kwa kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi pamoja na nia ya Serikali ya Austria uongozi na Serikali ya Tanzania katika utekelezaji wa Mkakati Mahususi wa Nishati (National Energy Compact) unaolenga kupeleka umeme kwa watanzania wote ipo mwaka 2030 kupitia mpango wa misheni 300.
Kikao kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Kampuni ya Merl kimefanyika
katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Mjini Vienna nchini Austria na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania na Mwakilishi wa Kudumu nchini Austria Balozi. Naimi S. Aziz pamoja na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Innocent Luoga.



Comments
Post a Comment