SERIKALI YADHAMIRIA KUITUMIA BAHARI KUKUZA UCHUMI WA BULUU
Na Mwandishi wetu
SERIKALI imesema imedhamiria kutumia rasilimali za bahari na maji ya ndani kwa maendeleo endelevu ya Taifa kupitia uchumi wa buluu.
Akifungua kongamano la kitaifa la wadau wa uchumi wa buluu leo Septemba 10, 2025 Jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu (Muungano) kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Abdallah Mitawi alisema uchumi wa buluu ni injini mpya ya maendeleo ya Tanzania.
"Uchumi wa buluu unaweza kuongeza ajira, biashara na kuboresha ustawi wa wananchi," alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchukuzi Shomari Shomari alisema maboresho ya bandari, reli na vyombo vya usafiri wa majini ni muhimu katika kuimarisha uchumi wa buluu na kuongeza ushindani wa kibiashara.
Naye Mkuu wa Chuo cha Bahari (DMI), Profesa Tumaini Gurumo alieleza kuwa chuo hicho kina jukumu la kutoa elimu, fanya utafiti na sekta ya bahari na mazingira ya pwani.
Kongamano hilo linafanyika kwa vikao vya Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Uchumi wa Buluu Zanzibar na DMI, likiwa na lengo la kusema kitaifa ya maendeleo ya uchumi wa dunia.





Comments
Post a Comment