SPEK KIWANDA HALISI CHA KITANZANIA CHENYE UWEZO MKUBWA MABOMBA




Na Mwandishi wetu

KAMPUNI ya  SPEK inayojiusisha na uzalishaji wa mabomba ambayo ni ya kizalendo imeendelea kung’ara katika sekta ya viwanda nchini kwa kuzalisha mabomba ya kisasa kwa ajili ya matumizi ya miradi ya maji, gesi na ujenzi.

Akizungumza Jijini Dar es salaam katika kongamano la Umoja wa wakandarasi na watoa huduma Shirikisho Tanzania (TUCASA) Ofisa Masoko wa kampuni hiyo amesema SPEK inajivunia kuwa kiwanda halisi cha Kitanzania, kilichoanzishwa kwa lengo la kutoa suluhisho la vifaa vya ujenzi na miundombinu ya maji na gesi, huku asilimia zote za umiliki zikiwa mikononi mwa Watanzania.

"Tunazalisha mabomba kuanzia ukubwa wa milimita 20 hadi 660. Mabomba haya yanatumika katika miradi ya maji yenye na isiyo na pressure, miradi ya gesi, na hata ujenzi wa kawaida," alisema.




Aidha, amesema wateja wao wakuu ni wakandarasi wa miradi ya Serikali kupitia mashirika kama RUWASA, pamoja na mashirika binafsi yanayoshiriki kutoa misaada ya miradi ya maji.

"Hatuachi nyuma wakulima, mafundi ujenzi wa kati na wakubwa, pamoja na wauzaji wa rejareja wa vifaa vya ujenzi. Tumekava sekta nzima," aliongeza.

Aidha amesema Kampuni ya SPEK pia imejipambanua kwa kuwa na teknolojia ya kisasa na maabara ya ndani ya kiwanda inayotumika kufanya uchunguzi wa ubora na usalama wa bidhaa zao, ili kuhakikisha mabomba yanayozalishwa yanaendana na viwango vya kimataifa na salama kwa matumizi ya wananchi.




Katika hatua nyingine aliwaalika  Watanzania wote wakiwemo wakulima, mafundi, wakandarasi na sekta binafsi kutembelea kiwanda chao ili kujionea teknolojia wanayotumia na namna wanavyohakikisha ubora wa bidhaa.


Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA