TMA YATOA MWELEKEO MSIMU WA MVUA ZA VULI OKTOBA HADI DESEMBA 2025

 



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema Mvua zinatarajiwa kuwa za Wastani hadi Chini ya Wastani katika maeneo mengi na kutawaliwa na vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko wa mvua usio na hakika hususan katika maeneo ya pwani ya kaskazini na Nyanda za Juu Kaskazini.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 11, 2025 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC) Dkt. Ladislaus Chang'a wakati akizugumza na Waziri wa habari kuhusu mwelekeo wa msimu wa mvua za Vuli (Oktoba hadi Disemba 2025), katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

“Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Oktoba, 2025 katika maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mara na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma na kusambaa maeneo ya pwani ya kaskazini na nyanda za juu kaskazini mashariki mwa wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Novemba 2025. Mvua zinatarajiwa kuisha mwezi, 2026,” amesema Dkt. Changa.

Dkt. Chang'a ametoa wito kwa wananchi taarifa za utabiri wa saa24, siku 10, mwezi na tahadhari zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ikizingatiwa kuwa mwelekeo wa mvua uliotolewa ni kipindi cha msimu wa miezi mitatu, hivyo viashairia mwenendo wa mambo ya mvua na mabadaliko ya muda mfupi utazingatiwa uchambuzi katika utabiri wa muda mfupi na mfupi. 

“Mvua za Vuli zinatarajiwa kuongezeka kidogo mwezi wa Desemba, 2025 na Vipindi vya joto kali kuliko kawaida vinatarajiwa katika msimu huu wa Vuli,” aliongeza Dkt. Changa

Aidha, Dkt. Chang'a amesema kuwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imeendelea kutoa taarifa za utabiri wa msimu mahususi kwa ngazi ya Wilaya.Wilaya 86 zilizo katika ukanda unaopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka zitapatiwa utabiri huo wa maeneo.

Msimu wa Mvua za Vuli ni mahususi kwa maeneo ya kaskazini mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro), pwani ya kaskazini (kaskazini mkoa wa Morogoro, mikoa ya Pwani (ikijumuisha maeneo ya Mafia), Dar es Salaam, Tanga pamoja na maeneo ya Unguja na Pemba), ukanda wa Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mkoa wa Pwani ya Pwani), pamoja na Mkoa wa Pwani ya Pwani, Unguja na Mkoa wa Pwani ya Pwani), pamoja na Mkoa wa Pwani ya Pwani, Unguja na Pwani ya Pwani ukanda wa Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mkoa wa Pwani) pamoja na kaskazini-mashariki.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA