WATU 10 WATIWA MBARONI KWA KUTUMIA NAMBA ZA SSH 2530 KINYUME NA SHERIA



Na Mwandishi Wetu

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu 10 kwa tuhuma za kutumia namba za magari zenye maandishi ya SSH 2530 kinyume na sheria.

Tukio hilo ni sehemu ya msako unaoendelea kufuatia agizo la Jeshi la Polisi lililotolewa kupitia kwa Msemaji wake, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) David Misime, aliyepiga marufuku matumizi ya namba hizo baada ya Septemba 1,2025.

Akizugumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mapema leo Septemba 4,2025 Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Jumanne Muliro, amesema kuwa operesheni hiyo inaendelea na watu zaidi wanaotumia namba hizo  wanatafutwa.

“Wale waliokamatwa walikutwa wakitumia namba hizo kwenye magari yao, jambo ambalo ni kinyume na sheria. Tunaendelea na msako ili kuhakikisha hakuna mtu anayevunja sheria hii kwa makusudi,” alisema Kamanda Muliro.

Amesema kwa mujibu wa Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168 (Marejeo ya mwaka 1973, yaliyofanyiwa marekebisho mwaka 2023), mtu yeyote anayeendesha gari bila usajili halali anatenda kosa la jinai.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA