WATUMISHI WIZARA YA NISHATI WAPATIWA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.





Ni baada ya Dkt.Biteko kuwakabidhi majiko yanayotumia umeme kidogo (Induction Cookers).


 Yaelezwa kuwa majiko hayo yanatumia umeme kidogo kwa gharama ndogo


Na Mwandishi wetu 


WATUMISHI wa Wizara ya Nishati  wamepata elimu ya matumizi bora na sahihi ya majiko yanayotumia umeme kidogo ( Induction cookers) baada ya kukabidhiwa maji hayo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko hivi karibuni.

Dkt. Biteko aliwakabidhi majiko hayo Watumishi wa Wizara ya Nishati ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia na kutambua kuwa Watumishi hao ni mabalozi katika utoaji wa elimu ya Nishati Safi ya Kupikia kwa wananchi.





Mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati- Mtumba, Dodoma yameandaliwa na Kitengo cha Nishati safi ya kupata matokeo na wataalam kutoka Kampuni ya Positive Cooker.

Akitoa elimu ya matumizi bora na sahihi ya majiko hayo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Positive Cooker,

Atukuzwe Willson ameeleza kuwa lengo la utoaji wa mafunzo hayo ni uhamasishaji wananchi kutumia ujumbe kwa kutumia kupitia majiko janja yanayotumia umeme kidogo.



"Lengo kutoa la elimu hii ni kulinda kila Mtanzania anaachana na lengo la matumizi yasiyosafi ili kulinda mazingira pamoja na afya zetu lakini pia ni sehemu ya msaada za kuunga mkono kampeni ya nishati safi ya kuleta hadi temothukiso mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania kutumia nishati ya kupikia. Amesema Willso





Mawasiliano kuhusu majiko hayo janja ya umeme amesema yanatumia wastani wa nusu uniti hadi uniti moja na nusu kwa wastani wa dakika 15 hadi dakika 90 sawa na shilingi 65 mpaka shilingi 534 tu hali inayothibitisha ufanisi wa majiko hayo kuwa na gharama nafuu, kuokoa muda, kulinda afya pamoja na mazingira.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA