ZIARA YA KAMPENI YA MGOMBEA URAIS WA NLD YATIKISA MKINGA

 




Na Mwandishi wetu, MKINGA TANGA 

Mgombea urais kupitia Chama cha NLD, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho,  Doyo Hassan Doyo, ameendelea na ziara yake katika kampeni katika Wilaya ya Mkinga, mara baada ya vyombo rasmi vya kampeni za uchaguzi.


Akiwa katika kanisa iliyofanyika kijiji cha Mtimbani na Moa, Doyo aliwahutubia wananchi na kusisitiza kuwa wakazi wa ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi wamesahauliwa na serikali iliyopo madarakani. 


Aliwaomba kwambapo watampa ridhaa ya kuongoza nchi, atahakikisha ananunua meli kubwa zitakazosaidia wavuvi na vijana wa hilo kupata ajira, sambamba na kufungua vituo vya uhamisho wa samaki ndani ya Wilaya ya Mkinga. “Pamoja na hali ngumuyopitia, bado nyavu zenu mnachomewa badala ya kuwekewa mazingira mazuri ya miti.Mkinipa ridhaa, nitahakikisha viwanda vya kusindika samaki vinajengwa katika ukanda huu ili vijana wapate ajira na kuuza bidhaa zao, kama samaki, kwa fedha za kigeni,” alisema Doyo.


Kwa upande wake, Meneja wa Kampeni wa kuleta Ibrahimu kuleta huyo, Ndugu Pogora Pogora, aliwataka wananchi wa Mkinga kutumia nafasi ya uchaguzi huu mabadiliko, akibainisha kuwa kosa si kufanya mabadiliko, bali ni kuridhika na maisha magumu yanayozidi majuto. "Tunawaomba wananchi msifanye makosa. Ili heshima yenu irudi, ni lazima kuleta mabadiliko kupitia kura zenu. Mpeni kura zote Mhe. Doyo ili aweze kupokea changamoto zenu," alisema Pogora.


Kampeni za Chama cha NLD zinaendelea, ambapo baada ya mkutano wa leo Mkinga, msafara wa kampeni unatarajiwa kuelekea Wilaya ya Muheza na baadaye Korogwe.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA