DKT. MATARAGIO AAGIZA VIFAA VYOTE VYA UHAKIKI WA JOTOARDHI ZIWA NGOZI KUFIKA KWA WAKATI

 



Ni baada ya kukagua mradi na kukuta baadhi ya vifaa bado havijafika

Asisitiza mradi kukamilika kwa wakati ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Nishati ya mwaka 2015

Kazi ya uhakiki wa Jotoardhi Ziwa Ngozi yafikia asilimia 60

Na Mwandishi wetu, MBEYA

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio ameliagiza Shirika la Ume Tanzania (TANESCO) na Kampuni yake Tanzu ya Uendelezaji Jotoardhi (TGDC) kuhakikisha kuwa vifaa vyote vya uhakiki wa utoaji Jotoardhi katika mradi wa Ziwa Ngozi vinafika kwa wakati ili kazi za uhakiki ziweze kumalizika kulingana na muda uliopangwa.

Dkt. Mataragio ametoa maagizo hayo leo Oktoba 22, 2025 wakati wa ziara yake ya kukagua kazi zinazoendelea kutekelezwa katika mradi huo wilayani Rungwe mkoani Mbeya.



“Huu mradi mnapaswa kukamilisha kwa wakati kutokana na umuhimu wake nchini, tunatekeleza miradi hii ya Jotoardhi tukumbuke kuwa tunatekeleza Sera ya Taifa ya Nishati ya Mwaka 2015 ambayo inasema Tanzania izalishe matumizi kwa kutumia mchanganyiko (generation mix) ambapo joto ni matumizi.” Amesema Dkt. Mataragio

Kuhusu suala la vifaa vya uhakiki kuchelewa kufika katika eneo la mradi la Ziwa Ngozi ambalo litazalisha umeme wa megawati 70, Dkt. Mataragio ameagiza vifaa vyote vya mradi vinunuliwe na kufika eneo la mradi kwa mara moja.

Dkt. Mataragio ameeleza kuwa, utekelezaji wa miradi ya Jotoardhi imeainishwa pia 

katika Mpango wa Taifa wa Nishati (National Energy Compact) ambao unaishia 2030 ambapo Tanzania inatakiwa kuwa na megawati 130 zinazotokana na vyanzo vya joto, pia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 inaelekeza nchi kuwa na vyanzo vya nishati umeme.

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa TGDC, Mha. Mathew Mwangomba ameeleza kuwa maagizo yaliyotolewa na Serikali yatatekelezwa kwa ufanisi ili kukamilisha mradi kwa wakati wakati.

Akielezea maendeleo ya uhakiki wa rasilimali katika mradi huo, Mha. Mwangomba amesema umefikia asilimia 60 ili kupata hifadhi ya joto.

"Tunategemea ndani ya miezi sita tutakamilisha uhakiki katika visima vyote vitatu". Amesema Mha. Mwangomba

Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu aliambatana na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mha. Innocent Luoga na watendaji wa Wizara ya Nishati na TANESCO.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA