DOYO : ATETEA HAKI NA AJIRA ZA WAANDISHI WA HABARI TABORA
Na Mwandishi wetu,TABORA
MGOMBEA urais kupitia Chama cha NLD, Doyo Hassan Doyo, akiwa katika ziara ya kampeni mkoani Tabora, amegusia sekta ya habari huku akibainisha changamoto wanazokabiliana nazo waandishi wa habari. Mhe. Doyo alieleza kuwa baadhi ya waandishi hawana ajira ya kudumu au mikataba thabiti katika mashirikiano yao ya habari, jambo ambalo si sahihi.
Doyo ameahidi kuwa, iwapo atapata ridhaa ya wananchi, atahakikisha analinda na kutetea maslahi mapana ya vyombo vya habari na waandishi katika kutekeleza uhuru wa habari na utendaji wao. Aidha, atasimamia kuhakikisha waandishi wanapata ajira rasmi na za kudumu.
Alisema ilani ya Chama cha NLD imezingatia makundi yote na kuainisha namna ya kutatua changamoto zao. Ilani hiyo, amesema, ni ya kizalendo kwani inabeba tunu za uzalendo, haki na maendeleo kwa kila Mtanzania. Mhe. Doyo pia alisisitiza kuwa hakuna chama kingine kilichojumuisha maoni na changamoto za Watanzania kwa uwiano katika ilani zao kama ilivyo Chama cha NLD.

Comments
Post a Comment